Ilikua ibada njema na ya furaha kwa wakazi wa Mtaa wa Mabwepande hapo jana. Katika Kanisa la K.K.K.T Mtaa wa Mabwepande lililochini ya Usharika wa Kijitonyama. Wazee wapya walioteuliwa kusimama katika nafasi ya wazee wa mtaa huo, Waliwekwa wakfu na kuingizwa kazini na Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama Mchungaji Daniel Mbowe akishirikiana na Mwinjilisti Kamnde wa Mtaa huo jana waliongoza ibada hiyo walipowaaga wazee wa kipindi kichopita wa kuwakaribisha wazee wapya. Ibada hiyo pia ilihudhuriwa na kwaya ya Uinjilisti toka sharikani Kijitonyama pamoja na kwaya ya Uinjilisti ya Mtaa huo. Waliipamba ibada hiyo.
Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama
Sehemu ya wazee walioteuliwa na washarika waliofika ibadani jana.
Kwaya ya Uinjilisti Mabwepande.
Wakati wa Neno Mchungaji Daniel Mbowe akihubiri
Kanisa lilifurika watu wengine wakaa nje.
Mzee aliyemaliza wakati wake akipokea zawadi ya cheti cha utumishi mwema.
Ndugu Eliasi Mboya akisoma neno.
Mchungaji Daniel Mbowe akiwaombea na kuwaweka wakfu wazee wapya walioteuliwa
Mwinjilisti Kamnde akisoma neno
Maombi yakiendelea
Kama wanavyoonekana wakati wa zoezi zima la kuwekwa wakfu wazee hao
Sehemu ya nje ya Kanisa hilo
Ndugu Kuttyferra aliteuliwa kusoma neno
Anociata Holela akisoma neno
Mchungaji Daniel Mbowe akiweka wakfu gari la Mwinjilisti Kamnde
Mwinjilisti Kamnde na familia yake wakizindua gari lao.
Gari hili limezinduliwa kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, AMEN
Bwana Mungu abariki kuingia kwenu na kutoka kwenu tangu sasa na hata milele. Ibada ikaisha hivo