Jumapili iliyopita
tarehe 29-07-29-2014. Kama ilivyo ada ya Jumapili za mwisho wa mwezi
usharikani Kijitonyama huwa na ibada ya Kusifu na Kuabudu na Maombezi.
Ibada ya wiki iliyopita ilikua ya tofauti yenye kujaa nguvu za Mungu
ndani yake. Ibada iliongozwa na Mchungaji Kiongozi wa Usharika Prosper
Kinyaha akishirikiana na Mwinjilisti Leonard Kipingu pamoja na Mtumishi
wa Mungu John Sembatwa aliyehubiri habari za Kuhuishwa na kutengenezwa
upya lakini akisisitiza habari za kusamehe na kuachilia mambo uliyowahi
kutendewa. Fuatana na mwandishi wa habari hizi katika picha hapo chini.
Praise Team wakishirikiana na Mtumishi wa Mungu Mwangosi (anayepiga keyboard) pamoja na wanamuziki wakiongoza washarika katika kuabudu.
Akina dada wa Praise Team wakiabudu
Akina kaka wa Praise Team wakiabudu
Kipindi cha sifa mambo ya Zambe wa Moyo!
Kanisa lilifurika sana watu walijaa, Kama wanavyoonekana wakijiachilia mbele za uwepo wa Mungu.
Kanisa likiwa limefurika watu mpaka ghorofani, Katika Ibada ya kusifu na kuabudu iliyofanyika siku hiyo.
Wengine walikosa mahali pa kukaa ndani ya kanisa, kama wanavyoonekana wakiwa kwenye hema lililokuwa nje ya kanisa.
Watu mbali mbali walimtolea Mungu shukrani zao za pekee kwa mambo makuu waliyotendewa, Mmoja wapo akiwa Grace Kaaya na binti yake (Waliopiga magoti Kulia).
Mchungaji Prosper Kinyaha, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa K.K.K.T Kijitonyama akisema neno la Ukaribisho kwa Mtumishi wa Mungu John Sembatwa ambaye ndiye alihubiri siku hiyo.
Mtumishi wa Mungu John Sembatwa akiwa katika mahubiri.
Mchungaji Prosper Kinyaha na Mwinjilisti Leonard wakitoa neno la shukrani kwa Mtumishi wa Mungu John Sembetwa.