Katika ibada iliyofanyika jana katika Kanisa la K.K.K.T Kijitonyama. Ikiongozwa na Mchungaji Msaidizi wa usharika wa Kijitonyama Mch. Prosper Kinyaha akisaidiana na Bw. Onai Seng'enge aliyekua kiongozi wa ibada hiyo na Petro Zakayo ambaye ndiye alikuwa mhubiri.
Jumuiya Maalum (Ebenezer) al maarufu kama Jumuiya Mchanganyiko kwa
umoja wao wakiwa wameshikilia jahazi la ibada hiyo jana waligusa nyoyo
za wajane kwa kutoa sadaka ya Vyerehani vinne pamoja na vifaa vyote vya
ushonaji kwa kundi la akina mama wajane wa usharikani hapo. Akisoma
risala Bw. Daudi Goodluck Daudi Alisema wameguswa kufanyanya hivyo ili
kuinua kipato cha akina mama hao. Aidha alisema takribani milioni moja
na nusu zilitumika katika upatikanaji wa vifaa.
Matukio katika picha:
Bwana Onai Seng'enge akiwa madhabahuni akiongoza Ibada.
Mchungaji Prosper Kinyaha Mchungaji Msaidizi wa Usharika wa Kijitonyama
Mchungaji Prosper Kinyama akiwaombea watu walikuja kumshukuru Mungu kwa shukrani za Pekee
Aliyewekewa mikono mkono wa kulia ni kijana Francis Malya (Macha)
Kwaya ya Jumuiya Maalum wakimtukuza Mungu wakati wa ibada
Bi Everlight akiongoza jahazi la kwaya ya Jumuiya Maalum.
Kijana wa Jumuiya Maalum akisoma neno la Waraka
Kijana wa Jumuiya Maalum akisoma neno la Mahubiri
Mwanadada huyu wa Jumuiya Maalum akisoma matangazo ya Usharika
Petro Zakayo akihubiri
Mchungaji Ernest Kadiva, Mchungaji Kiongozi wa Usharika wa Kijitonyama akitoa salamu.
Bwana Daudi Goodluck Daudi Mwenyekiti wa Jumuiya Maalum akisoma Risala ya Jumuiya yao Mbele ya washarika.
Sehemu ya wana Jumuiya Maalum wakisikila kwa Makini wakati wa ibada.
Maelfu ya watu waliofika kuabudu K.K.K.T Kijitonyama jana.
Sehemu ya sadaka kwa wajane iliyotolewa na Jumuiya Maalum
Tokea kulia mtu wa pili na wa tatu wakiwa wamejitokeza kuchangia sadaka kwa wajane
Bi. Margaret Kamugisha akitoa tangazo juu ya Uchangiaji wa Huduma ya kupeleka Injili kusikofikika utakaofanyika katika Hotel ya Land Mark Ubungo tarehe 30/03/2014 Kuanzia saa nane Mchana.
Usikose mtu wa Mungu.
Mwenyekiti wa Jumuiya Maalum Bw. Daudi Goodluck Daudi Akikabidhi kwa Mch. Ernest Kadiva, Sehemu ya vyerehani vinne pamoja na vifaa vya ushonaji vilivyotolewa zawadi kwa wajane wa Usharika wa Kijitonyama.
Waonaonekana na nyuso za furana ni akina mama wajane wa Usharika wa Kijitonyama wakifurahia zawadi toka kwa Jumuiya Maalum baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo na Mch. Ernest Kadiva.
Hivi ndivyo ibada ilivyoisha kwa maombi ya pamoja.