TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU ZANZIBAR KULAANI MASHAMBULIZI NAMAUAJI YA VIONGOZI WA DINI PAMOJA NA KUPINGA KAULI ZA UCHOCHEZI DHIDI YAZANZIBAR
Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mtukufu Mlezi wa Viumbe. Sala na salamu zimfikie Mtume wetu Mtukufu Muhammad (S.A.W), jamaa zake, maswahaba zake waongofu na wote wanaowafuata kwa wema hadi Siku ya Malipo.
Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar lililokaa Jumapili tarehe23/2/2013 katika kikao cha kutathmini matukio ya kushambuliwa na kuuliwaviongozi wa Dini yakiwemo ya karibuni ya kupigwa risasi na kuuliwa Padri Mushipamoja na kupigwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu waMwakaje na kuendelea kutolewa kwa kauli za uchochezi dhidi ya Zanzibarlinatamka ifuatavyo:
1. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani vikali na kwa nguvu zote matukio ya kushambuliwa na kuuliwa viongozi wa Dini likiwemo tukiola karibuni la kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi kulikofanywa na wahalifu wasioitakia mema Zanzibar.
2. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linapenda kuweka wazikuwa uhai ni tunu kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu aliyotunukiwa binaadamu hivyohakuna mwenye mamlaka ya kuiondoa haki hiyo isipokuwa yeye mweyewe Mwenyezi Mungu. Kutokana na ukweli huu ndio maana Sheria za Kiislamu zimeweka wazi mtumwenye kumuuwa mwenziwe naye auliwe kama inavyoelezwa katika Kitabu kitufu chaQuran kama ifuatavyo:
“Na humo (katika Taurati) tuliwaandikia ya kwamba mtu (huuwawa kwa sababu yakuuwa mtu) kwa mtu, ……….” (5:44)
Hivyo, vitendo vya kiharamia vya kushambuliwa viongozi wa Dini kulikoanziakwa kumwagiwa tindi kali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda, kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi nakushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu wa Mwakaje kwa dhulma kulikofanywa na wahalifu ni jambo lisilokubalika na Uislamuna Waislamu wenyewe. Aidha wahusika wa matendo haya wawe wafuasi wa Dini yoyoteile bado watahesabika ni wahalifu kwani vitendo vya kihalifu na kiharamia kamwehaviwezi kunasibishwa na Dini fulani.
3. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombo husika kufanya upelelezi wa kina kuhusu matukio haya kwa kuzingatia uadilifu namisingi ya kazi zao ili kuwabaini wahalifu na kufikishwa katika vyombo vyakisheria. Aidha Baraza linavitahadharisha vyombo hivyo kuepuka kufanya kazi yaokwa kusukumwa na matashi binafsi, jazba, chuki, matashi ya baadhi ya wanasiasana viongozi wa Dini pamoja na shindikizo la baadhi ya vyombo vya habari.
4. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani na kupingakwa nguvu zake zote kauli aliyoitoa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania nabaadhi ya vyombo vya habari kuihusisha Zanzibar na ugaidi kutokana na tukio la kuuliwa Padri Mushi. Kauli hii inaonesha kuwa Mheshimiwa Waziri anaibagua Zanzibar katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu tunavyoelewa sisi suala la usalama wa nchi ni suala la Muungano hivyo huwezi kuihusisha Zanzibar pekee na suala la ugaidi. Hivyo, Baraza linaona kuwa kauli hizi zinazotolewa ni mbinu za makusudi za kuichafua Zanzibar katika Jumuiya ya Kimataifa kutokana na chuki binafsi dhidi ya Zanzibar na watu wake.
5. Aidha Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linamtaka Mheshimiwa Waziri kwa kulinda heshima yake kuwajibika kwa Watanzania kwa kujiuzulu kutokana na kushindwa kulinda usalama wa wananchi wakiwemo viongoziwa Dini ambao ndio walezi wa jamii.
6. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linalaani kauli za uchochezi zinazoendelea kutolewa na baadhi ya vyombo vya habari zinazochochea chuki, uadui, hasama na mtafaruku kati ya Waislamu na Wakristo na kusahau kuwa Waislamu wameishi na Wakristo kwa amani, mapenzi na mashirikiano hapa Zanzibar karne na karne. Baraza linaona kuwa vyombo hivyo vya habari vinatekeleza ajenda ya kuivuruga Zanzibar kwa kuchochea vita vya kidini ili kufikia malengo yao wanayoyajua wenyewe. Hivyo, Baraza linaiomba Serikali kuvidhibiti kwa kuvichukulia hatua vyombo vyote vinavyotumia matukio haya kuchochea uadui na chuki kati ya Waislamu na Wakristo.
7. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaviomba vyombo vya habari vya Zanzibar kuwajibika kwa Wazanzibari wanaolipa kodi kwa kuwapasha taarifa sahihi juu ya matukio muhimu yanayotokea katika jamii yao badala ya wananchi kutegemea kupokea taarifa za upotoshaji na uchochezi kutoka katika vyombo vya habari visivyotutakia mema.
8. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linaziomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar kuwasilisha kwa Watanzania taarifa ya wazi ya matokeo ya uchunguzi wa matukio haya kwa kuanzia na lile la kumwagiwa tindi kali Sheikh Soraga, kupigwa risasi Padri Ambrose Mkenda, kuuliwa Padri huko Musoma, kupigwa risasi na kuuwawa Padri Mushi nakushambuliwa kwa mapanga na kuuliwa Sheikh Ali Khamis Bin Ali Khatibu waMwakaje.
9. Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar linawaomba Wazanzibari wote kuwa watulivu katika kipindi hichi ambapo upelelezi wa matukio haya ukiendelea. Aidha Baraza linawasihi Wazanzibari wote bila ya kujali tofauti zao za kidini kulinda umoja wao na kudumisha amani pamoja na kukataa kugawanywa ilikuwatoa katika ajenda yao ya msingi ya kudai Mamlaka Kamili ya Zanzibar katika Muungano.
MOLA WETU MTUKUFU TUNAKUOMBA UINUSURU ZANZIBAR NA WATU WAKE DHIDI YA MAADUI WANDANI NA NJE WASIOITAKIA MEMA NCHI YETU
Imesainiwa na:
Sheikh Ali Abdalla Shamte
Amir wa Baraza la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Zanzibar
MESSAGE
MESSAGE
Pages
Wednesday, February 27, 2013
Tuesday, February 26, 2013
Maznat Bridal Care Kuazimisha miaka 10 ya utendaji kazi
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Maznat
Bridal Care bi Maza alisema. Tarehe 5 May 2013 itakuwa ni siku maalum ya kuadhimisha
miaka 10 ya Maznat Bridal Care.Sherehe
hizo zitafanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubliee uliopo Dar es Salaam. Kampuni yake ambayo imekuwa ikijishughulisha
na urembo na upambaji wa maharusi, katika upambaji wa nywele za maharusi wa kike, kusafisha kucha n.k
Katika kipindi cha miaka kumi tangu mwaka 2003 mpaka mwaka
huu ameshapamba maharusi zaidi ya 10,000 ambao ni watu wa vipato vya aina
tofauti tofauti kuanzia wale vipato vikubwa iikiwa ni pamoja wale wasio kuwa na
nguo za harusi aliweza kuwapamba na kuwapa nguo harusi bure. Katika idadi hiyo ningependa wafike
walau maharusi wa kike 800 tu ambao walipambwa na salon yangu wakati wa sherehe
au harusi zao.
Siku hiyo watakuwepo wajasiriamali wane wakionesha bidhaa
zao ambao tungependa wainuke na kuwa wajasiriamali wakubwa kabisa wakianzia
chini na hatimaye kutimiza ndoto na matamanio yao. Matamanio ya Maznat Bridal
Care kwa wajasiriamali washuhudie kwamba ukinia inawezekana, ili mradi uwe
umejipanga na pia uwe mwaminifu kwa Mungu na kwa watu pia. Wito we tu ni “If
You Can Dream it, You Can do it’’ Kama unaweza kuwa na ndoto za kufanya kitu,
Unaweza kukifanya. Tutazindua Health andBeauty Workshops (Semina za Afya na
Urembo) zitakazokuwazikifanyika mara 2 kwa mwaka katika mikoa ya Dar es Salaam,
Morogoro, Arusha na Mwanza.
Kwa upande wa burudani, zitakuwepo za muziki kwa watu wa
aina zote, Atakuwepo mzee Yusufu, Bahati Bukuku, The Voice na THT.
Katika kuhakiki siku inapendeza kutakuwa na sare maalum ya kitenge toka Ghana kwa kila mgeni atakayefika ukumbini hapo, atapaswa kuwa amevalia sare hiyo. Kitenge hicho kitapatikana ukinunua tiketi yako mapema
Aidha siku hiyo zitatolewa zawadi mbali mbali kwa maharusi ambao
walipambwa na salon yake, zawadi hizo zitawalenga wale ambao wamesha zaa watoto
watatu katika kipindi cha mwaka 2003 hadi 2009 na wawe wanaweza kuvaa nguo
walizovaa siku za harusi zao (Shela) na ziwakae vizuri pia wawe na na picha za
nguo hiyo ikionekana vizuri walipozivaa siku ya harusi.
Pia zawadi nyingine za (shela) 3 zenye thamani ya shilingi za kitanzania laki
9 kila moja zitatolewa kwa bibi harusi watarajiwa, ambao watanunua tiketi
maalum na kufanyiwa mchakato na ndipo wataibuka maharusi watatu tu na kupewa
zawadi hizo.
Hii ni sehemu ya mapokezi kama inavyoonekana kusheheni bidhaa za mapambo ya nywele
Christian Bloggers wakisikiliza kwa makini maelezo toka kwa mmiliki wa salon ya Maznat Bridal Care
Sehemu ya duka upande wa maua ya aina mbali mbalimbali kama yanavyoonekana kwenye display cabinet
Duka la vifaa vya upambaji wa maharusi lililopo eneo la salon hiyo
Katika duka hilo pia zinapatikana nguo za maharusi wa kike ( Shela)
Waandishi wa habari za blog za kikristo (Christian Bloggers)
wakiwa wamepozi katika picha ya pamoja
Christian Bloggers wakitembelea duka hilo
Wednesday, February 6, 2013
KIJITO KWAYA ZIARANI KKKT KITUNDA RELINI
Kwaya ya Unjilisti imefanya ziara ya kiinjili katika kanisa la K.K.K.T Kitunda Relini kwa Mch. Ibrahim Gibore walipofanya huduma ya kusifu na kuabudu katika ibada iliyoandaliwa na usharika huo. Wakihudumu pamoja na kwaya wenyeji za usharika huo. Waliipamba ibada kwa sifa moto na kuabudu kulikosababisha uwepo wa Mungu kushuka katika ibada hiyo. Aidha katika ibaya hiyo alikuwepo mwanamuziki wa injili Upendo Nkone aliyehudumu ibadani pia. Somo la siku hiyo lilikuwa wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana Kondoo kama lilivyohubiriwa na Mch. Ibrahimu Gibore.
Haya ndiyo yaliyojiri katika picha
Aliyeshika kipaza sauti ni Katibu wa kwaya ya Uinjilisti Kijito Bw. Manyiga akitoa salamu za kwaya kwa washarika, kushoto ni Mchungaji wa usharika Ibrahimu Gibore wa Usharika wa Kitunda Relini.
Tokea shoto ni Allen Mwaipaja pamoja na Modest Mogan wakiwa kiroho zaidi wakati wa kipindi cha kuabudu wakati wa ibada
Dada Upendo Nkone akiwa amewainua watu juu kwa sifa
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa upako wa sifa ulipowashukia wana wa Mungu
Jopo la wanamuziki wa kwaya ya Uinjilist Kijito, Tokea kushoto Ni Jacob Mwaipaja akishughulika na gitaa la solo akifuatiwa na Micah Songo yeye akililazimisha gitaa la solo kutoa sauti kwa ustadi na anayefuatia ni Petro Mwampashi akiliungurumisha gitaa lenye mvumo mkuwa la bass
Fundi mitambo Lukio Mjema kama kawaida yake ni kuhakiki Sound imekaa vizuri
Sehemu ya umati wa washarika waliofika kuabudu kanisani hapo siku hiyo
Kijana Michael Piniel akikipapasa kinanda huku pembeni mwake MC Foma foma akishindwa kujizua kwa upako uliomshukia. Alikuwa kiroho zaidi
Kwaya wakiwa katika hali ya kuabudu na kuuita uwepo wa Mungu
Sifa inapokolea mambo huwa design hii
Haya ndiyo yaliyojiri katika picha
Aliyeshika kipaza sauti ni Katibu wa kwaya ya Uinjilisti Kijito Bw. Manyiga akitoa salamu za kwaya kwa washarika, kushoto ni Mchungaji wa usharika Ibrahimu Gibore wa Usharika wa Kitunda Relini.
Tokea shoto ni Allen Mwaipaja pamoja na Modest Mogan wakiwa kiroho zaidi wakati wa kipindi cha kuabudu wakati wa ibada
Dada Upendo Nkone akiwa amewainua watu juu kwa sifa
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa upako wa sifa ulipowashukia wana wa Mungu
Jopo la wanamuziki wa kwaya ya Uinjilist Kijito, Tokea kushoto Ni Jacob Mwaipaja akishughulika na gitaa la solo akifuatiwa na Micah Songo yeye akililazimisha gitaa la solo kutoa sauti kwa ustadi na anayefuatia ni Petro Mwampashi akiliungurumisha gitaa lenye mvumo mkuwa la bass
Fundi mitambo Lukio Mjema kama kawaida yake ni kuhakiki Sound imekaa vizuri
Sehemu ya umati wa washarika waliofika kuabudu kanisani hapo siku hiyo
Kijana Michael Piniel akikipapasa kinanda huku pembeni mwake MC Foma foma akishindwa kujizua kwa upako uliomshukia. Alikuwa kiroho zaidi
Kwaya wakiwa katika hali ya kuabudu na kuuita uwepo wa Mungu
Sifa inapokolea mambo huwa design hii
Subscribe to:
Posts (Atom)