Wapenzi wa K-junior Blog, Ni siku nyingine tena ya jumapili, kama kawida yetu huwaletea vipindi vya ibada inayofanyika kanisa la K.K.K.T Kijitonyama. Leo ilikuwa ni siku ya vijana hivyo ibada nzima iliongozwa na vijana. Ambao pia walijumuika pamoja na kwenda hospitali ya Mwananyamala kutoa huduma ya kugawa vitu kama Sabuni, Maji ya kunywa, Dawa za meno n.k. Pia kuadhimisha siku hiyo vijana walikusanyika pamoja kwa chakula cha mchana, Yafuatayo ni baadhi ya matukio ya siku hiyo katika picha.
Kwaya ya uamsho ndio walitufungulia dimba
Kwaya ya vijana wakafatia kumsifu Mungu
Judith Munisi yeye alisoma neno.
Abel Dilunga (a.k.a Gadi) Yeye alisoma matangazo
Mtui (wa kwanza kulia) Leo alikaa high table a.k.a patakatifu pa patakatifu. Akiwa na mzee wa kukwea pipa Mwinjilist Kipingu
Wadau Emmanule Sameji na my wife wake leo walitoa shukrani kwa mtoto wao Daniela kufikisha mwaka mmoja
Wakipata baraka toka kwa mtumishi wa Mungu mwinji Kipingu
Wadau wengine kibao walikuwepo kuwasindikiza
Wakati wa sifa, duh! wacha we kisouth africa zaidi. Kitu cha Solly Mahlangu. Emmanuel kikitawala sifa
Praise Team ya Kijito on the stage
Wakati wa worship watu wakazama rohoni
Praise Team wakimwandaa Mhubiri wa leo
Huyu ndiye aliyetulisha chakula cha kiroho leo
Wazee wa kanisa wa leo, wakifurahia jambo baada ya kumaliza ibada