Ilikuwa juzi jumapili, Harambee kubwa ya kutafuta fedha kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya ibada ya umoja wa makanisa ya C.C.T katika chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro. Harambee hiyo ilifana sana ikiongozwa na mgeni rasmi Prof. Josephat Kuzilwa akishirikiana na msaidizi wake Prof. Kamuzola. Pia kupambwa na kwaya mbalimbali mbali zilizokuwepo siku hiyo ikiwa ni pamoja na wenyeji kwaya ya U.C.F, Kwaya toka Mazimbu na kwaya toka Dar-es- Salaam Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama. Bila kusahau mshereheshaji wa shughuli hiyo alikuwa ni MC Shibanda wa Mwashibanda wenyewe wanamwita mzee wa haki ya Mungu.
Mambo yalikuwa kama ifuatavyo:
Hili ndilo jengo ilipofanyika ibada hiyo ikifuatiwa na harambee
Kwaya ya wenyeji wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe inayojulikana kwa jina ya U.C.F
Walipendeza sana huku wakiiteka mioyo ya wasikilizaji waliokuwepo katika ibada hiyo
Ni wazuri kwa steps na kucheza kama wanavyoonekana kwenye picha hapo juu.
Katika mtazamo mwingine wakiwa humbled
Prof. Kuzilwa akiongozwa kwaya yake jukwaani, Huyu prof. Yuko talented you cant believe MC Shibanda anasemaga 'Haki ya Mungu'
Katika mwonekano mwingine walitokelezea ki hivi
Kwaya ya Uinjilisti wakiwa wameliteka jukwaa kwa nyimbo za mapambio
Hapa wakicheza style yao ya kupiga gitaa wakiongozwa na mwana mama MJ
Drummer Boy Moses a.k.a Zinganoo akiipiga drums kwa umahiri
Kijana Michael hakusita kukipapasa kinanda kikatoa sauti za kuvuti
Dr. Tuntufye Mwamugobole mzee wa magitaa yote, this tym akatoka na gitaa la rhythm
Micah Songo yeye alikamata gitaa la solo, Anapiga gitaa huyu mpaka mlio wa nyau anaweza kukupigia
M.C Onai ye aliamua kutoka na tumba
Hii ndivyo high table ilivyosheheni wahshimiwa, Wachungaji na mgeni rasmi wa harambee
Mchungaji aliyehubiri akihamasisha watu kutolea Mungu kwa moyo katika ujenzi wa nyumba ya Mungu
Mwenyewe M.C Shibanda aliyekataa kuongoza shughuli mpaka avae koti kwanza
Hapa ni baada ya kulivaa koti na kuanza shughuli ya kusherehesha vema, ni kama anasema " Haki ya Mungu nimependeza"
M.C Shibanda akimkabidhi mgeni rasmi shughuli ya harambee huku akisisitiza mimi ni nani hata nisimame na mtu mzito kama huyu?
Prof. Kamuzola nae akajitokeza na kutamka dau lake katika kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mungu
M.C Foma foma akaomba kupiga picha na Prof. Huku akisema chance kama hizi zinatokeaga kwa nadra hivyo ukiipata itumie vema
Hawa ni kina dada wa kwaya ya uinjilisti wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhudumu
Mdau Tina (aliyesuka rasta) nae akaomba kutokelezea na rafiki yake kwenye blog
Hii ilikuwa ni ibada ya usiku wa jana yake jumamosi, wana U.C.F wakiwa jukwaani wakiimba nyimbo za Tenzi za Rohoni
Sifa zikavuma zikiongozwa na na mwanasifa wao
Upako uliposhuka watu wakajiachia mbele za Bwana
Hivi ndivyo walivyoonekana watu wote waliokuwepo kwenye Hall wakiabudu
Dada huyu wa kwaya ya uinjilisti Kijito anayefahamika kwa jina Jane aliwafurahisha watu kwa umahiri wake wa kuzipiga tumba
MESSAGE
MESSAGE
Pages
Tuesday, March 27, 2012
Monday, March 19, 2012
KWAYA YA HOSANA WAZINDUA ALBUM YAO
Jana ilikuwa siku ya furaha kwa Kwaya ya HOSANA C.C.T ya chuo kikuu cha Dar es Salaam, Pale walipozindindua Album yao Ijulikanayo kwa jina la UNITEGEMEZE. Iliyozinduliwa katika Ukumbi mpya wa UDSM. Iliyozinduliwa na mgeni rasmi bwana Msama. Wengi wanamfahamu kwa jina la Msana Promotions. Pia tamasha hilo la uzinduzi wa album yao lilisindikizwa na kwaya mbalimbali.
Album yenyewe ndo hii hapa
MC wa shughuli alikuwa Rita Chiwalo kama kawaida yake full kushagweka tu
Mchungaji Hiza akimkabidhi mgeni rasmi CD ili aweze kuizindua
MC Rita akimshirikisha jambo mgeni rasmi
Bonge George wa Mtoni Lulu akiwa na my wife wake wakipledge wakati wa uzinduzi
Bonge akizungumza jambo huku Joseph Msami na Rita Chiwalo wakimsikiliza
Haya wale wa enzi za mwalimu mnakikumbuka kiatu hiki? Hili kiatu alivaa Joseph Msami jana
Charles Tobias Malya nae alikuwepo kushusha ze upako
Wana Lulu mtoni wakijimwaga kwenye stage
The Rippers on the stage nao walikuwepo
Trinity Band wakionyesha umahiri wa kusifu Mungu
The Voice hawakukosa katika miondoko ya Acapela
Kijitonyama Uinjilisti wakijimwaya katika sebene la sifa
Hapa ni pale sebene lilipokolea admin akaweka camera chini na kuungana na wenzake na kuanza kucheza mbele za Bwana
Baadhi ya watu waliokuwepo katika ukumbi ambapo tamasha hilo lilifanyika
Hosana kwaya ambao ndio walikuwa wageni wa tamasha hilo la kuzindua cd yao mpya wakiwa stejini
Kwakweli walipendeza sana, tafuta cd yao mpya upate kuisikiliza
Subscribe to:
Posts (Atom)