Hakika hatuna budi ya kumshukuru Mungu kwa Mema mengi aliyotutendea kwa mwaka mzima uliopita wa 2011. Na sasa ni mwaka mwingine Mungu ametupa kuishi ndani yake. Omba kwa ajili ya mwaka huu mpya mapenzi ya Mungu yatimizwe kwako kwa mwaka huu, jiombee ulinzi wa Mungu uwe juu yako, Omba kwa ajili ya mafaniko yako binafi na familia yako pia.
MLEKYS na wadau wake wote tunakutakia heri ya mwaka mpya.
Baada ya salamu hizo nipende kukuletea matukio kadhaa yaliyojiri wakati wa kuukaribisha mwaka mpya katika kanisa la Kijitonyama KKKT, Nilipokuwa siku hiyo wakati tunausubiri mwaka mpya.
Hawa ni Kwaya ya Uamsho waliohudumu katika ibada ya tarehe 1 January 2012
wakiwa na furaha ya kuuanza mwaka mpya.
Na hawa ni Praise Team wakiimba huku wakimwandaa mtumishi aliyehubiri ibadani
Mchungaji Ernest Kadiva ndiye aliye hubiri jana, huku akisisitiza wakristo kuuanza mwaka na Bwana, Huku akisisitiza kuwa nio fedheha kwa mkristo kuuanza mwaka kwa tambiko na kwenda kwa waganga badala ya kumkabidhi Mungu maisha yao.
Kwaya ya Uinjilisti nao wakaamua kupiga picha ya pamoja baada ya Ibada wakimshukuru Mungu kwa kuingia mwaka mpya
Katika hali ya kupendeza huku mwaka ukiwa bado mbichi, Jengo la Kitega uchumi
la Usharika wa Kijito limefikia hali hii. Hebu ona linavyopendeza.
Hongera wanakijito kwa kazi njema ya Ujenzi
Hivi ndivyo linavoonekana kwa upande wa mbele.
Usiku wa kuukaribisha mwaka mpya wa 2012 huku ukiiagwa ule ulipita wa 2011
Kanisa la K.K.K.T Kijitonyama lilionekana katika mtizamo huu.
Watu wakiwa wamejaa mpaka nje jamani, walikuja kumshukuru Mungu kwa kuwalinda mwaka uliopita wa 2011. Hapa wakiwa katika ibada.
Shangwe, Vigelegele, Vifijo na Nderemo vilitawala baada ya saa sita kamili kufika
watu wakiselebuka mbele za Bwana baada ya kuingia mwaka mpya.
Uvumilivu ukawashinda watu wakaivamia madhabahu kwa raha huku wakimsifu Mungu na wimbo wa Hakuna Mungu Kama Wewe
Hawa nao wakifurahi kwa jinsi walivyoweza
Kanisa likiwa limefurika mpaka ghorofani
Wanamuziki waliohudumu usiku huo
Watu wakiwa wametaharuki wakiwa hawaamini wanachokiona kama kweli wameingia mwaka mpya wa 2012