MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Friday, December 30, 2011

ZIARA YA KWAYA YA UINJILISTI KIJITO MKOA WA KILIMANJARO

Ni hivi majuzi tu, tarehe 24 -27 Desemba 2011, Kwaya ya Uinjilisti ilifanya ziara yake mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi na Kufanya Tamasha kubwa la uimbaji ikiwa ni pamoja na kufanya huduma nyingine kadha wa kadha. Kama unavyojionea kwenye picha hapo chini.

Hii ilikuwa ibada ya usiku wa kuikaribisha Christmas, Kwaya walihudumu kwa njia ya uimbaji katika kanisa la KKKT Mjini Moshi

Tarehe 25 Desemba siku ya Christimas majira ya saa kumi jioni Kwaya ya uinjilisti walijumuika na wakazi wa Moshi katika Tamasha kubwa la uimbaji katika viwanja vya Uhuru Hotel zamani ikijulikana kama Uhuru Hostel, Na hivi ndivyo walivyoonekana wakiwa jukwaani wakisebeneka.
Ni wimbo wa Sifa kwako Bwana wangu ukiwa unatawala

Mambo yalipozidi kupendeza watoto nao hawakubaki nyuma katika kuonesha furaha zao za Christmas kama anavyoonekana mtoto wa mdau Mmbaga

Wakiwa katika hali ya kuabudu zaidi yimbo za aina zote ziliimbwa siku hiyo. Kwa waliokosa siku hiyo walikosa tamasha zuri sana.

Siku hiyo hiyo asubuhi walipata kusali katika Usharika wa Kiboriloni huku nako wakaimba kwa furaha na kuwaacha washarika wakiwa bado wana hamu ya kuendelea kusikiliza nyimbo zao.

Mdau aliyeshika mic ni MC Emmanuel Shedo akiwakaribisha watu kwenye tamasha lililofanyika baadae siku hiyo ya Christmas

Sehemu ya usharika waliosali siku hiyo ya Christmas kama kawaida wachagga wote walirudi nyumbani na kusababisha kanisa kufurika siku hiyo ya  siku kuu

Hawa ni baadhi ya wachungaji walihudumu siku hiyo katika usharika huo wa Kiboriloni

Mchungaji wa Usharika wa Kiboriloni akiwa katika kuhubiri

Tarehe 26 Desemba, Kwaya ya UinjilistI Kijito walikuwepo pia katika uzinduzi wa kanisa la usharika wa Rau wakiwa wamepwa mwaliko maalum na mlezi wa kwaya yao Bw. Hans Macha ambaye huo ni usharika wake wa nyumbani .

Washarika wakiwa nje huku shughuli ya uzinduzi ikiendelea, kanisa hili lilizinduliwa na Mh. Askofu Martin Shao kwa ushirikiano na askofu mkuu wa KKKT Askofu Alex Gehaz Malasusa akiwepo askofu mgeni kutoka sudani na wachungaji wengine.

Askofu kutoka Sudan akisoma neno wakati wa uzinduzi.

Jiwe la msingi linaonekana hivi.

Madhabahu ya kanisa ilionekana katika mtizamo huu siku hiyo.

Kwaya ya Uinjilisti Kijito waliketi kipande hii wakati wa ibada.

Washarika pamoja na jopo la wachungaji waliofika katika ibada hiyo.

Siku hiyo ilikuwa ni ibada maalum kwa ajili ya ubarikio wa watoto wa kipaimara, kama wanavyoonekana kwenye picha.

Maaskofu kwa utulivu wakisikiliza kwa makini wakati ibada ikiendelea, tokea shoto ni askofu toka Sudan jina hatukuweza kulipata wa pili ni Askofu Alex G. Malasusa na Askofu Martin Shao 

Hapa Askofu Martin Shao akimkabidhi hati maalum ya ushiriki mzuri wa ujenzi wa kanisa hilo Askofu mwenzake Alex G. Malasusa

Bwana Hans Macha nae akipokea hati yake.

Bwana Devis Mosha kwa Ushirikiano na Hans Macha waliongoza Harambee ya takribani milioni 80 na ushee, ikiwa ni gharama za kumalizia ujenzi wa kanisa hilo la Rau

Wakiwa wenye furaha walimtolea Mungu sehemu kubwa ya kiasi hicho 

Wazee wa Usharika wa Kijitonyama nao wakatoa ahadi zao, tokea kushoto ni Mr. Peniel Uliwa, Dr. Victoria Kisyombe, Mr. Noah Kadiva na Dr. Hans Macha

Waziri mkuu mstaafu Mh. Fredrick Sumaye nae alikuwepo siku hiyo.

Jioni yake kwaya walipata nafasi ya kumtyembelea mfadhili wao Bw. Devis Mosha huko nyumbani kwake Kiboriloni

Mtunza hazina wa kwaya Bw. Onai Seng'enge akizungumzia jambo wakati huo

Aminiel Mushi mmoja wa walimu wa kwaya akinena jambo pia

Wakaamua kupiga picha ya kumbukumbu pamoja na familia ya mfadhili wao.

Safarini kurudi Dar es Salaam kwaya walipita usharika wa Hedaru kujionea ujenzi wa kanisa ambalo walianzisha harambee ya ujenzi wake mwaka 2002  na hii ni hatua lilipofikia. Hongereni sana washarika wa Hedaru kwa kazi njema ya ujenzi wa nyumba ya Mungu. Hivi ndivyolinavyoonekana upande wa mbele.

Kwa upande wa nyuma linaonekana hivi.

Wenyeji wao wakisikiliza kwa makini kila kilichojiri.

Wakiwa na nyuso za uchovu wa safari  walisikiliza pia.

Kuimba ni jadi yao hawa watu, hawakuacha kuimba japo Hakuna Mungu Kama Wewe kwa wakazi wa Hedaru.

Katibu wa kwaya alipata muda wa kuongea neno na kuwashukuru.

Mtunza azina wa kwaya Bw. Onai nae hakukosa la kusema.

Katika safari nzima huyu Bw. hakukosa kuchukua japo vipande viwili vitatu vya ziara nzima nae si mwingine ni Gabriel Mniko wa GTV

Tuesday, December 20, 2011

Tangazo