MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, October 18, 2011

107.7 Upendo FM Radio Yatimiza Miaka Saba

Jana katika hafla iliyowakusanya wadau mbali mbali wa Radio hii, Wakiwa katika Usharika wa Kijitonyama.
Huku wakiwa na furaha tele kwa Radio hii kuwa na birthday yake ya saba tangu kuanzishwa kwake. Katika ibada iliyofanyika usharika huo iliyoongozwa na Mchungaji Ernest Kadiva aliyeshirikiana na Chaplain wa radio hiyo Mch.Moses Sozigwa aliyetoa historia fupi ya radio mahali ilikotoka na inakoelekea. Pia katika hafla hiyo walizindua mitambo yao ya OB (Outside Broadcasting). Pia sherehe hizo zilipambwa na kwaya mbalimbali na wasanii wa nyimbo za injili waliofika siku hiyo.
Angalia matukio katika picha. 

Hizi Frequency ambazo uki-tune unaipata Upendo Radio


Chaplain wa Radio Upendo Mch. Moses Sozigwa akinena jambo na wadau
Mwenyekiti wa Upendo FM Radio hakusita kutoa msisitizo


Mwenyekiti wa Upendo FM Radio akiwakaribisha wadau mbalimbali katika kujitolea kwa hali na mali kuichangia radio yao ya jamii


Kwaya ya Ebenezer kutoka Tabata nao walikuwepo kusherehekea Hepibesdei ya Upendo FM
Winners toka Ubungo KKKT nao walikuwa mstali wa mbele kabisa katika besdei ya U-fm


Mafundi mitambo walikuwa busy kuhakikisha matangazo yanarushwa hewani bila tatizo


Kwa hari na moyo watangazaji karibu wote walikuwepo kuhakiki usikivu mzuri wa radio


Mwanadada Martha Mwaipaja on the stage akiperfom


Perfomance haikuwa ya kitoto jukwaani ni baadhi ya watangazaji wa Radio Upendo wakishereheka kwa Upendo Radio kutimiza miaka saba ya kuwa hewani.


Ado Novemba na Utabaki kuwa Mungu, Aligusa nyoyo za wadau


Charles Tobias Malya uimbaji wake ulikuwa wa mvuto sana, alisherehesha pia.


Watangazaji wa Upendo Radio wakifurahia huku wakiwa na meneja wa radio 


Mama Agatha Lema Meneja wa radio akinena jambo na wadau katika kusherehekea 


MC Matemba ndiye aliyekuwa mshereheshaji mkuu wa siku hiyo


Vijana wa Kijitonyama nao walishiriki kwa ngonjela


Vijana wa Dar es Salaam Gospel Band walifanya makamuzi si kitoto


Hivi ndivyo walivyoonekana wakiwa stejini


Hawa ni watangazaji wa Upendo FM Radio kama ulikuwa huwajui


Watangazaji walikuja na familia zao katika kufurahia besdei


hawa pia ni watangazaji wa Upendo FM


Katika mtizamo mwingine walionekana hivi


Wachungaji hawa ni wadau wakubwa sana wa Upendo FM Radio tokea shoto ni Mch. Moses Sozigwa akiwa na Mch. Lewis Hiza


Mchungaji Hiza akiwa na my wife wake, hawa ni wadau katika kutoa vipindi vya ndoa katika Radio Upendo