Kwa mara nyingine tena, Kwaya ya uinjilisti Kijitonyama ilipata kusafiri kuelekea Tanga kwa huduma ya injili katika usharika wa Makorora.
Safari yao ilidumu kwa muda wa siku 2 kwani waliondoka Dar es Salaam siku ya jumamosi na kufanya huduma ya kuhamasisha harambee ya kumalizia ujenzi wa jengo la kanisa la Makorora siku ya jumapili.
Katika safari yao waliambatana na mkuu wa kanisa la KKKT Askofu Alex Malasusa
Ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika uhamasishaji katika harambee hiyo ambayo ilifana.
Hili ndilo basi walisosafiria hapa wakiwa wamefika njia panda ya Segera kupata japo soda |
Kama wanavyoonekana na uchovu kidogo wakisubiri soda ziletwe
Likiwa katika mtazamo mwingine ni gari walilosafiria
Hapa wakipata soda |
Tayari wamechangamka tayari kuendelea na safari
Kanisa ambalo walipokelewa kwanza kabla ya kufika Makorora
Kabla ya ibada hapa ilikuwa asubuhi kwaya wakikagua vyombo vyao kama viko salamabaada ya mvua kunyesha
Juhudi binafsi ilibidi zitumike ili kukausha maji kwa kila njia
Hatimaye mambo yakawa vema wakaanza injili kwa njia ya uimbaji
Wakiimba kwa sauti ambazo zilisababisha kuhamasisha watu kumtolea Mungu
Hivi ndivyo walivyojipanga stejini
Mpiga kinanda akiwa katika utumishi
Huyu nae akilipiga gitaa la solo kwa ustadi
Mwimbaji akiimba wimbo maarufu wa ndani ya safina (anayepiga gitaa)
Huyu ni kijana machachari katika kuzipiga drums
Tumba zilikuwepo pia kwa rahaaaa akionesha ustad wake kijana huyu
Baadhi ya wakristo walikuwepo katika ibada hiyo
Kwaya ya Tumaini Makorora wakimtukuza Mungu
Askofu Alex Malasusa akijadili na mkewe mama Erica Malasusa
Askofu akiwasikiliza wa waumini waliokuwepo ibadani siku hiyo
Tayari kabisa kupokea zawadi
Hapa akipewa zawadi ya msalaba anaye mvalisha ni dada wa kimasai
Askofu akivalishwa nguo za kimasai
Mama askofu naye akivalishwa nguo na urembo wa kimasai
Askofu akiifurahia zawadi