MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Wednesday, April 27, 2011

Ni Utumishi tu

Ijumaa kuu kwaya ya Uinjlisti kijito ilipata kuhudumu katika mkutano wa injili ulioandaliwa na kanisa la AICT Chang'ombe. Katika mkutano huo uliohudumiwa na mtumishi wa Mungu Isack. Mkutano ulifana sana kwani uliwarudisha watu wengi kwa Bwana Yesu. 

Mambo yalikuwa hivi: 

 Kwaya ikiwa katika huduma
 
Allen na Kelvin wakiongoza safina hiyo kati

 Safu ya wanamuziki tokea shoto Ni Jacob na Michael

 Kutifera na kinanda chake

 Mathew alishughulika  tumba

 Hapo sasa!

 Kazi ilikuwa ni kuimba na kucheza mbele za Bwana kama alivyofanya mfalme Daudi

 Dada Oliva akiongoza kundi katika uimbaji

 Kwaya ya wenyeji. A.I.C Chang'ombe wakiwa katika utumishi
 

Masanja Nae ni MPENDWA

Thursday, April 14, 2011

Ibada ya Kwaresma Kijito

Ikiwa imebaki wiki moja kabla ya siku kuu ya pasaka. Kama ilivyo ada ya usharika wa Kijito kuwa na ibada siku za jumatano kipindi cha kwaresma. Jana ibada hiyo iliongozwa na kwaya ya Uinjilisti ikiwa ni moja ya ratiba ya vikundi vya kwaya kuratibu ibada hizo kwa zamu. Ibada iliongozwa Na Joyce Nicholaus kwa ushirikiano wa Allen Mwaipaja ambaye ndiye alikuwa mhubiri na wazee wa zamu Godwin Manyiga, Modesta Mirisho na Suzan Mahenya. Pamoja na kwaya ya uinjilisti kwa ujumla ambao ndio walihudumu kwa njia ya nyimbo.
Fuatana nami katika matukio haya.

 Allen Mwaipaja akihubiri

  Joyce Nicholas ambaye ndiye aliongoza Ibada
 
 Sehemu ya wanakwaya wa kwaya ya uinjilisti walikuwe ibadani

 Upande mwingine wa wanakwaya

 Tokea kushoto niGodwin Manyiga, Suzan Mahenya na Modesta Mirisho
hawa ndio walihudumu kwa upande wa wazee wa zamu

 Sehemu ya washarika waliohudhuria ibadani


  Hivi ndivyo walivyoonekana watumishi wakiwa madhabahuni

 Kwaya wakihudumu kwa uimbaji

 Kiongozi wa ibada akiwaongoza watu kuomba

 Watumishi wakiwa "wamesimama kwenye zamu zao"

 Mtumishi huyo ndani ya joho. Utamjua?

 Mmmmh! Umeuvaa uhusika utadhani una experience ya miaka mingi
Mungu akubariki kwa utumishi wako wa jana.

 Wakiwa nje tayari kwa kumaliza ibada

 Enendeni kwa amani ya Bwana

 Wazee wa zamu wakiagana na kupongezana kwa utumishi


 Hongereni jamani! Zamu tumeimaliza

Wazee wa zamu wakiwa na watumishi katika picha ya pamoja

Tuesday, April 12, 2011

Mjengo wa Kitega Uchumi wa KKKT Kijito Wazidi Kupendeza

Jana katika pitapita zangu pale kanisani Kijito nilipoinua macho nikaona maendeleo mazuri ya ujenzi wa jengo hili. Sikuwa nimetembea na camera yangu. Bahati nzuri simu yangu ina camera nikaona ni vema niwashirikishe na nyinyi muone kazi nzuri ya wanakijito lakini pia mzidi kuwaombea katika kufanikisha hatua za mwisho za ujenzi huo. Mungu awabariki sana wana Kijito kwa moyo wenu wa kujitoa na kuomba.

 Linavyoonekana ubavuni

Huu ni upande wa mbele, 
Kama utaona vizuri sampling ya madirisha imeanza kuwekwa,
Na pia juu design ya uezekaji imeanza.

Monday, April 4, 2011

Yaliyojiri Kijito Wiki Iliyopita Katika Ibada Jumapili

Kwa mara nyingine tena Namshukuru Mungu aliyeniwezesha kupata matukio haya katika picha. 
Zifuatazo ni picha za sehemu ndogo ya ibada iliyofanyika katika usharika wa Kijitonyama KKKT. Ibada ilikuwa ya aina yake huku ikisindikizwa na vikundi mbali mbali vya kwaya ikiwemo Praise Team. Pia Mchungaji wa Usharika Kadiva akiwa na jopo la watumishi aliohudumu nao akiwemo Mwinjilisti Kipingu pamoja Mwinjilisti Mndeme ambaye ndiye alihubiri siku hiyo.

Fuatana nami katika picha.

 Praise Team wakiwaongoza washarika katika kuualika uwepo wa Mungu ibadani
wakimwandaa mhubiri wa siku hiyo kwa kusafisha hali ya hewa ya rohoni

 Kundi zima la Praise Team wakiabudu


 Allen na Kelvin wakiwa katika kuutafuta uwepo wa roho mtakatifu

 Kelvin Akiongoza worship

 Allen akiongoza worship

 Hivi ndivyo alivyoonekana Kelvin wakati wa kuabudu

 Allen naye alikuwa hivi wakati wa kuabudu
 Wanamuziki Wakiitenda kazi yao vema tokea kushoto ni Anord, Ully na Eugene


 Sehemu ya washarika wakiwa katika kuabudu

 Hawa ni Kwaya Kuu nao wakiabudu

 Mwinjilisti Mndeme akihubiri

 Tokea shoto ni Mwinjilisti Kipingu, Mwinjilisti Mndeme na Mchungaji Kadiva 
akitoa baraka kwa washarika wakati wa kumaliza ibada ya siku hiyo

 Sehemu ya washarika waliokuwepo wakati wa kumaliza ibada