MESSAGE


I made this widget at MyFlashFetish.com.

Tuesday, October 26, 2010

Mdau Orpah Ala Nondoz!

Juzi tarehe 24-10-2010, Dada yetu mpendwa Orpah alipata degree yake ka kwanza
katika mchepuo wa Education. Akiwa mwenye furaha pamja na marafiki zake baada
ya kuwa wametunukiwa shahada zao kama wanavyoonekana kwenye picha. Akiwe mama
mchungaji Mzinga akiwa naye amepata nondoz.




Monday, October 11, 2010

Obligado! (Thanks, Thank You)

Inapendeza Jamani. Sifa kama hizi zinabariki sana.

Friday, October 8, 2010

Haya Wale wakutendeleza Kazi kwenu.

Ni kibao kingine cha mwanadada Esther Wahome,
Hebu kione.

Monday, October 4, 2010

Hiii Nimeipenda

Nimeipenda hii nikaona bora niwamovuzishie na nyinyi muione hii,
nawatia moyo kina dada na kina mama na nyinyi mjifunze kutumia
vyombo vya muziki kama mama huyu!

Kitchen Party ya Stella


Chereko chereko na Heko heko zilisikika Jana katika ukumbi wa Hotel 92
Iliyopo maeneo ya Sinza Legho. Wakati dada Stella Munisi alipofanya Kitchen Party yake
Huku akisindikizwa na marafiki zake kibao.

Hebu ona Ilivyofana!


























Birthday

Juzi jumamosi Ilikuwa ni Happybirthday ya kuzaliwa kwangu!!!
Namshukuru Mungu aliyenijali nikaweza kuiona tena tarehe 2nd October
Kumbe ninazidi kula chumvi. Shukurani zimwendee Mungu wangu aliyenitunza
Kufikia siku hii. Kwani ni wengi walitamani kufikia umri wangu hawakuweza.
Ila mimi Mungu kanipendelea kwa neema tu.

Katika picha ndivyo ilivyokuwa birthday yangu.
Zawadi kemkem ziliandaliwa kwaajili yangu!


Hivi ndivyo ilivyokuwa keki waliyonizawadi wapendwa wenzangu
kabla haijaliwa
Hapa nikimlisha keki dada Joyce
Upande wa wanamuziki, Jacob Alikula kipande cha keki
Kata keki tule, kata keki tule ndiyo walivyokuwa wakiimba wakati huo nakata keki

Kisu juu tayari kwa kukata keki ya Birthday
Dada Leah akilishwa keki
Martha ambaye ndiye alikuwa MC wa hako ka hafla kafupi ndiye aliyenilisha keki

Kwaya ya Uinjilisti Katika Huduma ya UEM

Juzi Jumamosi kwaya ya Uinjilisti Ilipata kualikwa kuhudumu Katika Mkutano wa UEM
United Evangelical Mission Unaoendelea katika kanisa la KKKT Kunduchi.
Kwa muda watakriban wiki moja hivi.

Na haya ndiyo yaliyojiri katika picha.
Kweli kuimba ni raha jamani. Hebu waone hawa kina dada wanavyofurahi!

Mzee wa mpini wa solo Micah Songo akipigiwa makofi na mwanamuziki mwenzie!

Hiyo ni style maarufu kwa jina "twende kwa Yesu" Ona inavyochezwa!

Watoto wa Kijitonyama KKKT nao hawakubaki nyuma katima kucheza

Mambo ya ngonjela hayo. Wanafanya vizuri sana katika fani hiyo.
Hawa nao walikuwa wakimsifu Mungu kwa style zao!

Mmmmh! Palikuwa hapatoshi. Vijana hawa waliuteka umati wa watu kwa kucheza

Kijana Joshua akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma ya Kigogo
Kila mtu alikuwa anacheza kadri roho alivyomjalia


Walioshika nao kila mtu anaimba kwa hisia

Haya wale viongozi wa goma la asili ya kigogo Oliva na Mushi wakiimba kwa Hisia.

Safu ya Muziki nayo Ilikuwa imekamilika. Kwa karibu kijana machachari Kibambe Akizikwida ngoma kweli kweli!

Haya sasa vijana wakiwa kazini. Ni utumishi tu!

Kinadada wakiwa wamevaa vazi la asili la kigogo